1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Musharaff azuru makao makuu ya umoja wa Ulaya.

13 Septemba 2006

Rais wa Pakistan Pervez Musharaff ameutaka umoja wa Ulaya kuimarisha biashara na uwekezaji kuisaidia nchi yake kuweza kupambana na ugaidi, ambao amesema umeingizwa nchini humo kutoka nje.

Musharaff pia ameonya mataifa ya magharibi kuwa wapiganaji wa Taliban ni kundi baya zaidi la magaidi kuliko Al Qaeda kwasababu ya uungwaji mkono mkubwa wanaoupata miongoni mwa watu wa Afghanistan.

Kiongozi huyo wa Pakistan alikuwa akizungumza na wabunge wa umoja wa Ulaya katika ziara yake ya kwanza katika makao makuu ya umoja huo mjini Brussels.

Musharaff pia amesema pia kuwa anamatumaini juu ya nafasi ya kupata suluhisho la miongo kadha la mzozo kati ya India na nchi yake katika eneo la Kashmir.

Leo Musharaff anatarajiwa kukutana na mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW