1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Mzozo wa Umoja wa Ulaya

17 Juni 2005

Viongozi wa nchi 25 za Umoja wa Ulaya wamekubaliana juu ya kuongeza muda wa kuratibisha katiba mpya ya Umoja wao.

Hapo awali nchi wanachama zilitakiwa kuipitisha katiba hiyo hadi mwezi Novemba mwaka kesho.

Rais wa baraza la Umoja huo bwana Jean Claude Juncker ameeleza hayo baada ya siku ya kwanza ya kikao cha dharura cha viongozi wa Umoja wa Ulaya kinachofanyika mjini Brussels kutafakari mgogoro wa katiba.

Kutokana na uamuzi huo, Denmark na Ureno zimeahirisha kura za maoni juu ya katiba Umoja wa Ulaya kwa muda usiojulikana.

Hatahivyo viongozi wengi wanaunga mkono kuendelea kwa mazungumzo juu ya Uturuki kujiunga na Umoja huo .

Aidha Rumania na Bulgaria zitaweza kujiunga bila ya kuchelewa.

Leo kwenye mutano wao viongozi wa Umoja wa Ulaya watajadili njia za kutatua mzozo juu ya fedha za kugharamia umoja wao.

.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW