BRUSSELS :Poland yaonywa,inaweza kunyimwa fedha
20 Juni 2007Matangazo
Tume ya Umoja wa Ulaya imeionya Poland,kuwa huenda ikanyimwa fedha ikiwa itaendelea kuzuia kufikiwa mapatano juu ya kuleta mageuzi katika taasisi za Umoja wa Ulaya.
Viongozi wa nchi za Umoja huo wanatarajiwa kufanya mkutano kesho mjini Brussels kujadili mageuzi hayo.
Poland inataka mabadiliko yafanyike katika utaratibu wa kupiga kura ndani ya Umoja wa Ulaya ili kurahisisha mchakato wa kufanya maamuzi.
Poland imesema utaratibu mpya utazipa nchi kubwa kama Ujerumani usemi mkubwa zaidi.