BRUSSELS : Ulaya yamuunga Mfaransa kuongoza IMF
10 Julai 2007Matangazo
Umoja wa Ulaya umemchaguwa Strauss-Kahn wa Ufaransa kuongoza Shirika la Fedha la Kimataifa la IMF.
Ureno ambayo iliongoza mazungumzo kati ya mataifa yote ya 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya amesema Ulaya itamuunga mkono Srauss-Khan waziri wa fedha wa zamani wa Ufaransa baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa hivi sasa wa IMF Rodrigo Rato wa Uhispania kun’gatuka.
Katika tangazo la kushangaza mwezi uliopita Rato amesema ataachia wadhifa huo hapo mwezi wa Oktoba.