Brussels. Umoja wa Ulaya kutoa milioni 42 kwa Lebanon.
30 Agosti 2006Matangazo
Umoja wa Ulaya umesema kuwa utaidhinisha kutolewa kwa Euro milioni 42 kwa ajili ya juhudi za ujenzi mpya nchini Lebanon.
Kamishna wa masuala ya mambo ya nje, Benita Ferrero-Waldner, amesema mpango huo utawasilishwa rasmi katika mkutano wa kimataifa wa wafadhili mjini Stockholm siku ya Alhamis.
Kiasi kikubwa cha msaada huo kitakwenda katika kusaidia wafanyabiashara wa Lebanon kuweza kurejesha uwezo wao.