1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS Umoja wa Ulaya na Libya kushirikiana kuwazuia wahamiaji wasio halali

29 Juni 2005

Umoja wa Ulaya na Libya zitashirikiana kuwazuia wahamiaji haramu kutoka Libya kusafiri kwenda mataifa ya jumuiya hiyo. Rais wa halmashauri ya jumuiya ya Ulaya, Jose Manuel Barroso na kamishna anayehusika na maswala ya maendeleo, Louis Michel, watasafiri kwenda nchini Libya juma lijalo kujadili ushirikiano na serikali ya Tripoli na kuunda mikakati kadhaa ya kukabaliana na wahamiaji wasio halali.

Mipango itakayodumu kwa mda mrefu inajumulisha kutoa mafunzo kwa walinda usalama wa mipakani na polisi, na kuunda njia za kuwaokoa wahamiaji wanaokufa maji katika bahari ya mediterrenean, wakijaribu kuingia Ulaya.

Makamu wa rais wa halmashauri ya jumuiya ya Ulaya, ambaye husimamia maswala ya uhamaji, amesema kwamba visa vya kuhuzunisha vya wahamiaji kufariki dunia wakiwa baharini, lazima visiruhusiwe kutokea tena.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW