1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Umoja wa Ulaya una wasi wasi na msimamo wa Iran

7 Agosti 2005

Umoja wa Ulaya umesema utaunga mkono wito wa Marekani wa kutaka Iran ifikishwe kwenye Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwekewa vikwazo iwapo serikali ya Tehran itaanza tena shughuli za nuklea.

Hatua hiyo imekuja baada ya Iran kukataa pendekezo la Umoja wa Ulaya la kuipatia nchi hiyo vifuta jasho vya biashara na kisiasa ili isitishe shughuli zake za nishati ya nuklea.Umoja wa Ulaya umesema mapendekezo yake yanakusudia kuiruhusu Iran kuwa na teknolojia ya nuklea lakini kuzuwiya shughuli zake ambazo zinaweza kusaidia kutengeneza bomu la atomiki.

Rais mpya wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amesema hapo jana kwamba wakati Iran itaheshimu sheria za kimataifa haitokubali kutishwa.Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani ameelezea wasi wasi wake juu ya msimamo huo wa Iran wakati waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Philippe Douste –Blazy amewataka viongozi wa Iran kuyaangalia kwa makini mapendekezo ya Umoja wa Ulaya.

Nchi tatu za Umoja wa Ulaya Ujerumani,Ufaransa na Uingereza zimekuwa zikijaribu kutafuta muafaka kati ya Iran na Marekani juu suala la mipango ya nuklea ya Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW