1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Umoja wa Ulaya waeleza wasi wasi wake juu ya hali ya mashariki ya kati.

15 Julai 2006

Umoja wa Ulaya umeeleza wasi wasi wake kuwa mapigano katika mashariki ya kati yanaweza kusambaa hadi Syria, ambayo chama chake tawala cha Baath kimeeleza kuwa kinaunga mkono Lebanon dhidi ya kile inachokiita mashambulizi ya kinyama ya Israel.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amewasiliana na wenzake nchini Israel, Syria na Misr kujadili kuhusu mzozo huo.

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana anatarajiwa kwenda mashariki ya kati leo kwa mazungumzo juu ya mzozo huo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa amezungumza na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na kumtaka kuepuka kuwadhuru raia. Cyprus itaunga mkono uondoaji wa pamoja wa raia wa umoja wa Ulaya waliokwama nchini Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW