1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Umoja wa Ulaya wafurahia kuchaguliwa kwa kiongozi wa Cyprus ya Waturuki anayependelea mazungumzo ya muungano.

18 Aprili 2005

Umoja wa Ulaya umeufurahia ushindi wa Mehmet Ali Talat katika uchaguzi wa eneo la Waturuki huko Cyprus. Katika taarifa, tume ya Ulaya , imesema kuwa ushindi wa Bwana Talat utaharakisha kuanzishwa upya kwa mazungumzo ya muungano katika kisiwa hicho kilichogawika. Tume hiyo pia imesema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yataleta kuondolewa kwa hatua ya kuzuwia misaada ya jumuiya ya Ulaya pamoja na masharti ya biashara nafuu kwa eneo hilo la kaskazini ya Cyprus. Talat, ambaye amepata zaidi ya asilimia 55 ya kura, anapendelea kumalizika kwa mgawanyiko katika kisiwa hicho kilichoko katika bahari ya Mediterranean kupitia mazungumzo na upande wa Wagiriki wa Cyprus walioko upande wa kusini.

Anachukua nafasi ya rais Rauf Denktash, ambaye anastaafu baada ya utawala wake wa miaka 30 katika serikali iliyojitangaza ya jamhuri ya Cyprus ya kaskazini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW