1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya wajadili hali ya Darfur

15 Septemba 2006

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wamekutana leo mjini Brussels Ubelgiji kujadili mzozo wa Darfur.

Viongozi hao wameionya serikali ya Sudan na waasi wa Darfur kwamba watabeba dhamana kwa uhalifu unaondelea katika eneo hilo na kuzitaka pande zote mbili ziheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano.

Hata hivyo hawakusema ikiwa Umoja wa Ulaya utawasilisha kesi katika mahakama ya kimataifa ya jinai mjini The Hague, Uholanzi.

Mawaziri hao wamesema serikali ya Sudan ina jukumu la kuwalinda raia wake wote kutokana na mashambulio na kuheshimu haki za binadamu.

Pia wameutahadharisha ulimwengu juu ya kuendelea kuzorota kwa hali mbaya ya kibinadamu katika jimbo hilo la Darfur.

´Tuna wasiwasi mkubwa sana kuhusu kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu ya kutokuwepo njia ya wazi ya kisiasa ya kukituma kikosi cha Umoja wa Mataifa.´

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya pia wamezitaka pande zinazopigana ziruhusu misaada ya kiutu iwafikie waathiriwa wa vita huko Darfur.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW