1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Uturuki inaweza kujinga na umoja wa Ulaya kuanzia mwaka 20014.

30 Juni 2005

Umoja wa Ulaya umekubaliana kuhusu mpango wa mazungumzo kwa ajili ya uanachama wa Uturuki katika umoja huo. Haya yalifikiwa katika mkutano wa makamishna mjini Brussels.

Kufuatia mazungumzo hayo , kamishna anayeshughulikia upanuzi Olli Rehn amewaambia waandishi wa habari kuwa chini ya mpago huo , Uturuki inaweza kujiunga na umoja wa Ulaya kuanzia mwaka 2014.

Hii ni kutokana na bajeti ya umoja huo ya muda mrefu ambayo inaanzia mwaka 2007 hadi 2013.

Pia amesema kuwa Uturuki inahitaji kupita katika mageuzi sita ya kisheria kabla ya mazungumzo ya kujiunga na umoja huo kuanza kama ilivyopangwa hapo Oktoba.

Mazungumzo hayo yataachwa wazi, bila ya uhakika kuwa Uturuki itapatiwa nafasi ya uanachama.

Baadhi ya makamishna wenye imani kali za kidini, wamekuwa wakitoa hoja kwamba Uturuki nchi ambayo ina Waislamu wengi ipewe nafasi muhimu ya ushirika bila kuwa mwanachama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW