1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Misaada ya ruzuku kwa Afrika,Asia na Amerika Kusini

9 Januari 2004
Makao makuu yas Umoja wa Ulaya yameidinisha euro milioni 31.1 katika misaada ya ruzuku ya kibinaadamu leo hii ambapo sehemu kubwa ya misaada hiyo itakwenda Afghanistan kuwasaidia watoto wenye utapia mlo katika kipindi hiki cha majira ya baridi.

Tume ya Umoja wa Ulaya imesema katika taarifa kwamba miradi 14 iliopitishwa itatekelezwa na mashirika ya kibinaadamu yanayoendesha shughuli zao katika maeneo yaliokusudiwa.

Ziada ya euro milioni 6.27 kwa ajili ya Afghanistan na wakimbizi katika nchi jirani ya Iran na Pakistan miradi hiyo inajumuisha euro milioni 5.14 kwa ajili ya wakimbizi wa Sahrawi katika jimbo la Tindour nchini Algeria na euro milioni 5 kwa ajili ya kusambaza chakula kwa ajili ya watoto wa Korea Kaskazini.

Ethiopia na Somalia zitapata Euro milioni mbili na nusu kila mmoja kuwasaidia watu walioathiriwa na ukame na migogoro.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW