1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Mkutano wa viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya waendelea Brussels,Ubelgiji

17 Juni 2005

Viongozi wakuu wa umoja wa ulaya wanakutana mjini Brussels kwa siku ya pili kujadili suala nyeti la bajeti ya Umoja huo.

Kwenye kikao cha leo mada kuu inayotarajiwa kujadiliwa ni kuhusu nafuu ya mabilioni ya euro inayopokea Uingereza kutokana na mchango wake kwenye bajeti ya Umoja huo.

Hata hivyo Uingereza imesema italijadili suala hilo iwapo tu kiwango cha kikubwa cha ruzuku kwa wakulima wa Ulaya kitapunguzwa hatua ambayo inapingwa vikali na Ufaransa ambayo inafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na sera hiyo.

Mjadala huo kuhusu bajeti unakuja baada ya viongozi hao kukubaliana juu ya kuongeza muda wa kuidhiniasha katiba mpya ya Umoja huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW