BRUSSELS:Pascal Lamy mkuu mpya wa WTO
1 Septemba 2005Matangazo
Pascal Lamy amechukua rasmi wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa shirika la biashara duniani WTO.
Lamy mwenye umri wa miaka 58 aliyekuwa kamishna wa zamani wa umoja wa Ulaya amechukua nafasi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Supachai Panitchpakdi.
Hata hivyo Lamy anakabiliwa na majukumu mazito ikiwa ni pamoja na kuutatua mzozo wa kibiashara kati ya China na Marekani na Umoja wa Ulaya na China.