1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Uingereza na Poland kutumia kura ya turufu

21 Juni 2007

Ujerumani ikiwa mwenyekiti wa sasa wa umoja wa ulaya,
imeonya kwamba mazungumzo ya kuunda katiba mpya ya umoja huo yanaweza yakashindwa. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier akizungumza kabla ya mkutano wa kilele mjini Brussels amezitaka nchi wanachama kufikia maridhiano.
Poland na Uingereza zimeonya kwamba zinaweza zikatumia kura ya turufu , iwapo pingamizi zao hazita shughulikiwa katika hali ya kuridhisha.Poland inapinga vikali utaratibu wa upigaji kura uliopendekezwa na Ujerumani na Uingereza inataka
hakikisho kwamba misingi ya uhuru katika katiba mpya ya umoja wa ulaya haitaathiri sheria za Uingereza na pia inapinga kuteuliwa Waziri wa mambo ya nchi za nje
wa Ulaya.

Katiba mpya inatarajiwa kuchukua nafasi ya ile ilioshindwa na ambayo iliangushwa katika kura za maoni zilizopigwa Ufaransa na Uholanzi 2005.


Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW