1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Ulaya na kitisho cha homa ya ndege

17 Oktoba 2005

Mkuu wa Halmshauri ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso amesema Umoja huo lazima uchukue hatua kali za kinga,ili kuzuia usambazaji wa homa ya mafua ya ndege,lakini kwa wakati huo huo isizushwe hali ya khofu.Umoja wa Ulaya umepiga marufuku uingizaji wa mifugo kama kuku na bata kutoka Rumania na Uturuki,baada ya virusi vya homa ya ndege,aina ya H5N1 kuthibitishwa katika nchi hizo mbili.Ingawa ndege huambukizana virusi hivyo,ni shida kwa binadamu kuambukizwa.Lakini homa ya mafua ya ndege imeshauwa watu 60 katika nchi za Asia na maafisa wa tiba wana khofu kuwa virusi hivyo huenda vikabadilika na binadamu wakaja kuambukizana kwa urahisi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW