1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Ulaya,U.S zakubaliana kuwa na anga huru

22 Machi 2007

Waziri wa usafirishaji wa Ujerumani, Wolfgang Tiefensee amesema kuwa Umoja wa Ulaya kwa kauli moja umeunga mkono mpango wa kuwa na anga huru kati ya Ulaya na Marekani.

Wolfgang ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao cha mawaziri wa usafirishaji wa umoja huo, mjini Brussels, Ubelgiji hata hivyo amesema kuwa utaratibu huo utachelewa kuanza katika muda wa miezi mitano ijayo kutokana na ombi la Uingereza.

Mkataba huo umekubalika baada ya miaka minne ya mazungumzo, na utaruhusu ndege za kiraia za mataifa ya Umoja na Ulaya na Marekani kuruka katika anga za nchi hizo bila ya kikwazo chochote.