1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Umoja wa Ulaya wautaka Umoja wa Mataifa kuufanikisha uchaguzi mkuu wa Ivory Coast

20 Mei 2005

Umoja wa Ulaya umeutaka Umoja wa Mataifa kuchukua nafasi kubwa katika kuufanikisha uchaguzi wa Rais wa Ivory Coast utakaofanyika mwezi Oktoba.

Umoja wa Ulaya pia umeutolea mwito Umoja wa Mataifa utumie uwezo wake kuisaidia nchi hiyo katika mpango wake wa amani.

Taarifa iliyotolewa na rais wa sasa wa Luxenmbourg,inasema Umoja wa Ulaya umeyakaribisha maendeleo yalioyopatikana hivi karibuni nchini Ivory Coast na kuvitaka vyama vyote nchini humo kutekeleza wajibu wao bila kuchelewa.

Umoja wa Ulaya umewataka watu wa Ivory Coast kushirikiana kikamilifu na Umoja wa Mataifa kuhakikisha uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 30 mwezi Oktoba mwaka huu unafanyika bila Kuchelewa na bila matatizo.

Waasi na vikosi vya kijeshi walitia saini makubaliano jumamosi iliyopita ya kumaliza vita vilivyoigawanya nchi hiyo mara mbili , Kaskazini kwa waasi na kusini kwa upande wa serikali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW