BUCHAREST:Homa ya ndege barani Ulaya
16 Oktoba 2005Matangazo
Romania imetangaza hatua mpya baada ya ugonjwa wa homa ya ndege kuthibitishwa nchini humo.Hatua hizo ni pamoja na kuuwa kuku na mabata wote katika sehemu zenye ugonjwa huo.Rumania pia imepiga marufuku shughuli zote uwindaji na manyesho.
Msemaji wa serikali amethibitisha kwamba homa ya ndege iliyogundulika nchini humo ni sawa na ile iliyoua watu zaidi ya sitini katika nchi za Asia.
.Shirika la afya duniani WHO limetahadharisha juu ya hatari ya mamilioni ya watu kufa duniani kote ikiwa vijidudu vya ugonjwa huo vitabadilika na kuingia katika miili ya binadamu ambapo wataweza kuambukizana.