BUDAPEST: Nyota wa kandanda wa zamani, Ferenc Puskas afariki dunia
18 Novemba 2006Matangazo
Mwanasoka mashuhuri wa zamani kutoka Hungary, Ferenc Puskas, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79. Puskas, ameiaga dunia katika hospitali ya mjini Budapest alipokuwa akilazwa kwa magonjwa ya homa na mapafu. Puskas, alikuwa na hoda wa timu ya kandanda ya taifa ya Hungary ambayo haikuwahi kushindwa katika michezo 32 mfululizo kabla ya kupoteza mbele ya Ujerumani katika fainali za kuuwania kombe la soka la dunia la mwaka 1954.