BUJUMBURA: Bunge la Burundi lawaidhinisha makamu wawili wa rais
29 Agosti 2005Matangazo
Bunge nchini Burundi leo limewaidhinisha makamu wawili wa rais waliopendekezwa na rais Piere Nkurunziza kutoka kwa makabila mawili nchini humo. Bunge hilo lilimkubali Martin Nduwimana wa chama kikuu cha watutsi kama makamu wa rais wa kwanza na Alice Nzomukunda wa chama cha wahutu kuwa makamu wa rais wa pili.
Nduwimana wa chama cha UPRONA na Nzomukunda wa chama cha FDD watakuwa makamu wa rais Nkurunziza chini ya utawala wa kugawa madaraka kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo iliyoanza kufanya kazi mwezi Februari mwaka huu. Makamu wa kwanza wa rais atashughulikia utawala na wa pili atakuwa na jukumu la uchumi na maswala ya kijamii.