BUJUMBURA: Burundi yapata rais wa mpito
20 Agosti 2005Matangazo
Bunge jipya la Burundi limemchagua rais wa mpito wa nchi hiyo.Baadhi kubwa ya wabunge wamemchagua,Pierre Nkurunziza aliekuwa mtetezi pekee.Kuchaguliwa kwa Nkurunziza,aliekuwa kiongozi wa waasi wa Kihutu,ni sehemu ya hatua za mwisho za utaratibu wa amani wenye lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.Vita hivyo viliodumu miaka 12,vilisababisha mmuagiko mkubwa wa damu.Nkurunziza,siku ya Alkhamis katika hotuba yake,aliahidi kufanya kazi kuleta umoja na kumaliza mapigano kati ya Wahutu walio wengi na Watutsi wachache.