BUJUMBURA: Burundi yautaka umoja wa mataifa kushughulikia elimu na afya
9 Novemba 2005Matangazo
Serikali ya Burundi imesema umoja wa mataifa unatakiwa kuelekeza juhudi zake nchini humo kwa maswala ya elimu na afya mbali na kulinda amani. Msemaji wa serikali, bwana Karenga Ramadhani aliyasema hayo baada ya mkutano kati ya mawaziri wa Burundi na wajumbe wa umoja wa mataifa nchini humo.
Umoja huo unatakiwa kuongeza juhudi zaidi za amani katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ambako waasi wa Burundi waliokataa kufanya mazungumzo ya kutafuta suluhu, wanashirikiana na makundi yaliyojihami na silaha.