1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bujumbura: Rais Domitien Ndayizeye wa Burundi ameizuru maiti ya mjumbe ...

31 Desemba 2003

wa Vatikan askofu Michael Courtney aliyeuliwa jumatatu iliyopita mjini Bujumbura.Maiti ya askofu huyo aliyeuliwa kiwa katika juhudi za amani nchini Burundi imelazwa katika hospitali ya Prince Louis Rwagasore mjini Bujumbura.Itasafirishwa baadae hii leo kuelekea Ireland.Wakati huo huo wanamgambo wa kundi la FNL nchini Burundi wamesema hawahusiki hata kidogo na kuuliwa mjumbe huyo wa Vatikan. Forces Nationales de Libération FNL ni chama pekee kilichosalia cha waasi,kinachopigana dhidi ya serikali ya mpito.Jeshi la Burundi na mkuu wa maaskofu wa Burundi Mgr Simon Ntamwana wamekituhumu chama ahicho kuwa nyuma ya shambulio lililopelekea kuuwawa mjumbe huyo wa Vatikan. Msemaji wa FNL ,Pasteur Habimana analituhumu jeshi la Burundi kua nyuma ya shambulio hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW