1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA. Umoja wa mataifa walaani kurudishwa wakimbizi wa Rwanda

15 Juni 2005

Umoja wa mataifa umesema kuwa Burundi imevunja mapatano ya kimataifa ya haki za wakimbizi ilipo warudisha kwa lazima maelfu ya wakimbizi wa kinyaruanda waliotorokea nchini Burundi kwa hofu ya kufikishwa mbele ya mahakama za Gachacha nchini mwao.

Lakini waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Jean Marie Ngendahayo amekanusha madai hayo na kusema kuwa wakimbizi wa Kihutu wapatao 4,700 waliondoka kutoka kambi ya wakimbizi ya Songore iliyo kaskazini mwa Burundi kurudi nyumbani Rwanda kwa hiari yao.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan amesema kuwa wakimbizi hao walirudishwa kwa nguvu hivyo basikuilaumu Burundi kwa kukiuka mapatano ya umoja wa mataifa ya mwaka 1951 juu ya haki za wakimbizi na mapatano ya mwaka 1974 ya umoja wa nchi huru za Afrika.

Wanyaruanda hao walikimbilia nchini Burundi tangu mwezi wa 4 kwa hofu ya kutotendewa haki iwapo watafikishwa mbele ya mahakama za Gachacha.

Kuna habari kuwa watu 11 waliumia waliporuka kutoka kwenye malori yaliyokuwa njiani kuwapeleka wakimbizi hao katika mpaka wa Burundi na Rwanda.

Kurudishwa kwa wakimbizi hao kumefuatia serikali za Rwanda na Burundi kupitisha kuwa kuwepo kwao nchini Burundi ni kinyume cha sheria kwa sababu za kuwa usalama nchini Rwanda ni shwari.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW