1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA :Wanne wahukumiwa kifo kwa mauaji ya Manlan

4 Mei 2005

Mahakama ya Burundi imewahukumu kifo maafisa wanne waandamizi wa polisi kwa kuhusika na mauaji ya mwakilishi wa shirika la Afya duniani WHO nchini humo mnamo mwaka 2001.

Kassi Manlan aliuwawa na mwili wake kutupwa kwenye kingo za mto Tanganyika.

Maafisa hao wamehukumiwa kifo bila ya wao kuwepo mahakamani wakati maafisa wengine tisa wamehukumiwa vifungo kati ya miaka 2 gerezani hadi vifungo vya maisha.

Mahakama ya Rufaa nchini Burundi imewaona polisi hao wanne Emile Manisha,Gerard Ntunzwenayo,Japhet Ndayegamiye na Aloys Biziman kuwa na hatia ya kupanga mauaji ya Manlan juu ya kwamba wamekataa kukiri makosa hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW