Bujumbura:Chama cha waasi wa zamani wa Burundi, FDD, kimeshinda uchaguzi wa bunge
6 Julai 2005Matangazo
Kikundi cha waasi wa Kihutu wa zamani kimepata asilimia 58 ya kura katika uchaguzi wa bunge uliofanywa jumatatu iliopita huko Burundi. Baada ya kura kuhesabiwa, kamati huru ya uchaguzi ilihakikisha kwamba chama cha FDD kimepata wingi wa kura., Chama tawala cha Wahutu, kinachoongozwa na Rais Domitien Ndayizaye, kilichukuwa nafasi ya pili, kikipata asilimia 22 ya kura. Chama cha FDD kimesema kinataka kupamnana na umaskini na kuendeleza mapatano na maridhiano baada ya Burundi mnamo miaka 12 iliopita kujionea uhasama wa kikabila kati ya jeshi la taifa, linaloongozwa na Watuts, na waasi. Wabunge watachagua rais mpya wa nchi hapo Agosti mwaka huu.