BUJUMBURA:Rais Ndayizeye amfuta kazi waziri wake wa nishati na kumchagua mwengine
26 Mei 2005Rais wa Burundi Domitien Ndayizeye amemchagua Thaddee Nkanira kuchukua nafasi ya waziri wa nishati na madini bwana Andre Nkundikije aliyemtimua kazini kwa kile alichokitaja kuwa makosa makubwa.
Msemaji wa rais Ndayizeye Pancrase Cimpaye amesema mara kadhaa waziri huyo aliyetimuliwa alishindwa kutofautisha kati masuala yanayohusu wizara yake na masuala ya chama chake.
Nkundikije ambaye ni mwanachama wa kundi la kikabila la watsusti waliowachache na kiongozi wa chama cha Intwari amekuwa serikalini tangu mwaka 2002.
Serikali ya mpito pamoja na makundi ya waasi wa zamani na vyama vya kisiasa wanajitayarisha kuelekea katika uchaguzi wa urais mwezi Agosti tarehe 19.
Burundi imekabiliwa na vita vya kikabila kwa zaidi ya miaka 11 ambapo zaidi ya watu laki tatu wengi wakiwa wananchi wa kawaida waliuwawa kwenye mapigano hayo.