BUJUMBURA:Uhalifu wa kivita kuadhibiwa nchini Burundi
17 Juni 2005Matangazo
Serikali ya Burundi imeidhinisha mpango wa Umoja wa Mataifa juu ya kuunda tume ya usuluhishi na mahakama maalumu itakayohukumu kesi za uhalifu wa kivita.
Waziri wa sheria wa Burundi bwana Kiganahe amesema mpango huo wa Umoja wa Mataifa unawafiki dhamira ya watu wa nchi yake juu ya kuunda tume na mahakama zitakazowaadhibu watu waliotenda makosa.
Hatahivyo Umoja wa Mataifa bado haujapitisha mpango huo.
.