BUJUMBURA:Uhalifu wa vita kuadhibiwa nchini Burundi
17 Juni 2005Matangazo
Serikali ya Burundi imeidhinisha mpango wa Umoja wa Mataifa juu ya kuunda tume ya maridhiano na mahakama maalum itakayowahukumu wahalifu wa kivita nchini humo.
Tume hiyo ni sehemu ya mpango wa kumaliza mzozo wa miongo minne wa kikabila kati ya wahutu waliowengi na watutsi waliowachache.
Waziri wa wa sheria nchini Burundi Didace Kiganahe amesema mpango huo wa Umoja wa Mataifa unawafiki dhamira ya Warundi juu ya kuunda tume na mahakama zitakazowahukumu watu waliotenda makosa ya uhalifu wa kivita.
Hata hivyo baraza la usalama la umoja wa Mataifa halijaupitisha mpango huo.