1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bulgaria yapiga marufuku uhamasishaji LGBTQ+ skuli

8 Agosti 2024

Serikali ya Bulgaria imetangaza marufuku ya ujumbe wowote wenye maudhui ya mapenzi ya jinsia moja kwenye skuli, ikifuatia hatua kama hizo zilizochukuliwa na Hungary, Poland na Slovakia.

Waungaji mkono mapenzi ya jinsia moja wakiandamana Bulgaria.
Waungaji mkono mapenzi ya jinsia moja wakiandamana Bulgaria.Picha: Stoyan Nenov/REUTERS

Sheria mpya iliyotangazwa hapo jana inakataza ushajiishaji au matangazo yanayohusiana na kile kinachoitwa "mapenzi yasiyo ya kimaumbile" au kujitangazia jinsia isiyo sahihi kinyume na ile ya kuzaliwa kwenye skuli za chekechea na skuli za kawaida.

Uamuzi huu unaifanya Bulgaria kuwa nchi ya nne kwenye Umoja wa Ulaya kupiga marufuku masuala hayo.

Soma zaidi: Papa Francis: Naelewa upinzani wa kubariki ushoga Afrika

Mabadiliko hayo ya sheria yaliyoanzishwa na chama cha Vazrazhdane, kinachoelemea Urusi, yaliungwa mkono pia na makundi mbalimbali ya kisiasa bungeni, kikiwemo chama cha mrengo wa kati kulia, Gerb-SDS.

Makundi yanayounga mkono wapenzi wa jinsia moja waliandamana mbele ya majengo ya bunge hapo jana yakipinga kupitishwa kwa sheria waliyodai inafuata "njia ya Urusi."