1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga huenda ikabaki bila mashabiki hadi 2021

28 Agosti 2020

Mechi za ligi kuu ya kandanda Ujerumani - Bundesliga huenda zikabaki bila mashabiki hadi mwaka ujao baada ya Kansela wa Angela Merkel kutangaza kuwa zuio la mikusanyiko mikubwa litarefushwa hadi Desemba 31

Fußball Bundesliga FC Schalke - VfL Wolfsburg
Picha: Getty Images/AFP/W. Rattay

Mechi za ligi kuu ya kandanda Ujerumani - Bundesliga huenda zikabaki bila mashabiki hadi mwaka ujao baada ya Kansela wa Angela Merkel kutangaza kuwa zuio la mikusanyiko mikubwa litarefushwa hadi Desemba 31.

Merkel alikutana na magavana wake 16 wa majimbo Alhamisi kujadili jinsi ya kusonga mbele shughuli za kila siku wakati maambukizi ya virusi vya corona yakipanda tena Ujerumani.

Michezo haikuwa mada kuu ya mazungumzo hayo, lakini inahusika na uamuzi wa kurefusha marufuku dhidi ya mikusanyiko ambayo usafi na ufuatiliaji haviwezi kuhakikishwa.

Marufuku hiyo awali ilistahili kumalizika Oktoba 31 lakini imerefushwa kwa miezi mingine miwili.

Wakuu wa magavana wa majimbo wataunda kikundi cha kuzingatia uwezekano wa watazamaji kuhudhuria hafla na kuripoti matokeo yao ifikapo mwishoni mwa Oktoba.

dpa

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW