1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUNDESLIGA NA KOMBE LA KLABU BINGWA ZA AFRIKA

Ramadhan Ali14 Agosti 2006

Bundesliga-Ligi ya Ujerumani na Kombe la Klabu bingwa barani Afrika zilikuwa uwanjani mwishoni mwa wiki.Mashindano ya ubingwa wa riadha ya ulaya yalimalizika kwa Russia kuparamia kileleni na bingwa mpya wa ringi ya mabondia ya WBC ni Oleg Maskaev.

Bremen yatamba kwa mabao 4:2 dhidi ya Hannover
Bremen yatamba kwa mabao 4:2 dhidi ya HannoverPicha: AP

Bundesliga:Ligi ya Ujerumani, mabingwa Bayern Munich na mahasimu wao wakubwa katika kinyan’ganyiro cha taji msimu huuWerder Bremen-wote wawili walianza uzuri pale firimbi ilipolia mwishoni mwa wiki kuanzisha msimu mpya.Munich ilianza vyema kwa kuizaba Borussia Dortmund mabao 2:0 katika Allianz Arena wakati Bremen, ilitoka nyuma jana na mwishoe, kuipiga kumbo Hannover kwa mabao 4:2.

Mahasimu wengine wakubwa wanaoania taji Schalke na Hamburg walipatwa na mkosi kila mmoja katika azma yao ya kuivua taji Bayern munichj.

Hamburg, iliomaliza watatu msimu uliopita ,ilibidi kuridhika na suluhu ya bao 1:1 katika mpambano wake na Armenia Bielefeld.Schalke nayo ikazimwa pia kwa bao 1:1 na Eintracht Frankfurt.

Katika lango la Bayern Munich alilinda tena nahodha Oliver Kahn, ambae katika Kombe la dunia aliwekwa kando na kocha Jürgen Klinsmann aliependelea kumuona Jens Lehmann kipa wa Arsenal bora kukaa langoni.Oliver kahn alicheza mpambano wake wa 500 wa Bundesliga siku hiyo na alitamba langoni .

Akiwa amestaafu lakini katika timu ya Taifa, lango la Ujerumani litalindwa tena na Jens Lehmann keshokutwa jumatano pale Ujerumani itakapotimiza miadi yake na Sweden,katika marudio ya changamoto yao ya Kombe la dunia.Huo lakini, utakua mpambano wa kirafiki.

Ujerumani pia itacheza bila ya nahodha wake Michael Ballack alieumia akiichezea timu yake mpya Chelsea ya Uingereza.Chelsea ilizabwa mabao 2:1 na Liverpool katika mpambano huo.Kocha mpya wa Ujerumani, Joachim Low,aliechukua usukani kutoka kwa Klinsmann anatumai hatahivyo, kuwa Ballaci atakua fit kwa changamoto ya kwanza ya ujerumani na Ireland hapo Septemba 2 kuania tiketi ya finali za Kombe la Ulaya la mataifa, 2008 nchini Uswisi.

Huko Holland,Ajax Amsterdam, imetwaa Kombe la Super Cup nchini baada ya kuwalaza mabingwa PSV Eindhoven.

Mwishoni mwa wiki, ilikua pia zamu ya kinyan’ganyiro cha vikombe 2 vya Afrika-kombe la shirikisho la dimba –CAF na kombe la klabu bingwa-champions League:

ASEC Abidjan ya Ivory Coast,iliitimua Enyimba ya Nigeria kwa mabao 3:0 na hivyo imekata tiketi ya nusu-finali ya kombe hilo kutoka kundi B.

Mabingwa watetezi,Misri walimudu sare tu 0:0 na wenyeji Asante kotoko huko Obuasi,Ghana.

Katika kundi A, CS Ffaxien ya Tunisia iliondoka na ushindi wapili kwa kuizaba JS Kabylie ya Algeria bao 1:0.

Katika kinyan’ganyiro cha Kombe la Confederations Cup-kombe la shirikisho la dimba la africa,mabao 4 mnamo dakika 15 za mwisho yalitosha kwa St.Eloi Lupopo kuizaba Renancimientto ya Guinea ya Ekweta na kuitoa kwa mabao 5:1.

Etiole du Sahel ya Tunisia iliwaslaza mahasimu wao wa mtaani Esperence kwa bao 1:0.Katika mpambano kati ya timu mbili za Angola mjini Luanda, Petro Atletico imeilaza InterClube pia ya luanda mabao 3:1 .Duru ya pili ya kinyan’ganyiro cha kombe hili itachezwa August 26-27.

Mashimndano ya riadha ya ubingwa wa Ulaya yalimalizika jana rasmi mjini Gothenburg, Sweden,huku Russia, ikiibukwa kileleni dola kuu la riadha barani Ulaya:

Wakati mashindano haya yatakumbukwa kwa ushindi wa mataji 2 ya mreno wa asili ya Nigeria,Francis Obikwelu katika mita 100 na 200 na ule wa mbelegiji Tim Gevaert wa masafa hayo upande wa wanawake, Urusi imeibuka kileleni mwa orodha ya medali kwa medali 12 za dhahabu,12 za fedha na 10 za shaba kutoka michezo 47.Ujerumani ilikuja wapili kwa medali 4 za dhahabu,3 za fedha na 2 za shaba.

Muamerika,mzaliwa wa Kazakhstan, Oleg Maskaev ametwaa taji la 3 mwishoni mwa wiki, alipomdengua Hasim rahman kwa mara nyengine tena kama alivyofanya 1999.Bingwa mpya kwahivyo wa taji la WBC ni Oleg Maskaev aliemzima Hasim rahman katika dakika ya mwisho ya duru ya 12.

Kwa ushindi wa Maskaev ,mataji yote 4 sasa yamo mikononi mwa mabondia wa asili ya Uruisi ya zamani-(Soviet Union).Wakati Maskaev, anahodhi mataji 3 ya wezani wa juu, muukraine Wladmir Klitschko, anaedhibiti taji la 4 la IBF.Sasa medani ni wazi kwa wababe hawa 2 kupambana ili ama Klitcho anavaa mataji 3 ya Maskaev au Maskaev anachukua la 4 la Klitchko na kuandika historia ya mabondia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW