Bunge Cyprus, kupigia kura ya uokozi
18 Machi 2013Hatua hiyo inayotarajiwa sasa itafikiwa baada ya mjadala mrefu ulioahirishwa mara kadhaa kwa lengo la kufanikisha mashauriano kuhusu suala hilo tata.
Wiki iliyopita katika mkutano wake uliyofanyika Brussels, kanda inayotumia sarafu ya euro ilikadiria kiasi cha euro bilioni 10 ikiwa sawa na dola za kimarekani bilioni 13 kwa lengo la kukikwamua kiuchumi kisiwa hicho kilichopo katika bahari ya Mediterranean.
Makato yanayolaumiwa
Wanaoweka fedha zao katika mabenki watakabiliwa na makato fulani ya kodi. Kwa mfano mwenye kiasi cha mpaka euro 100,000 watatozwa kiasi cha asilimia 6.75 na zaidi ya akiba hiyo kiwango cha tozo kinaweza kufikia mpaka asilimia 9.9.
Mpango huo wa fedha za uokozi ulikuwa upigiwe kura jana, lakini baadae alasiri ukaahirishwa mpaka leo hii. Rais Nicos Anastasiades wa Cyprus ameonya pasipo fedha hizo sekta ya kifedha ya taifa hilo itaporomoka, na kulitupungiza taifa katika mkwamo wa kiuchumi kwa kufirisika kabisa.
Matumaini finyu ya kupitisha mkopo
Kiongozi huyo anaungwa mkono na viti 28 kati ya viti 56 vya bunge la taifa hilo ambalo kwa uamuzi wake unatorajaiwa unaelezwa, unaweza kuliondoa taifa hilo katika mkwamo.
Hata hivyo vyama viwili vya upinzani AKEL na EDEK vimemekwisha sema haviungi mkono mpango huo wa uokozi kutoka kanda inayotumia safari ya euro.
Katika hatua nyingine iliyochukuliwa mwishoni mwa juma mabenki yamezuia akanuti za wafunga akaunti za wateja wao ile ya kawaida pamoja na ya njia ya mtandao kwa lengo la kuzuia wateja wenye hasira kuchukua fedha zao katika mabenki kutokana na kukasirishwa na mapendekezo hayo.
Urusi yalalamikia mpango wa kanda ya euro
Kwa kawaida jumatatu ni siku ya mapunziko kwa shughuli za kibenki, benki zote zinafungwa nchini Cyprus lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo serikali itaendelea kuzifunga taasisi zake za fedha hata kesho kwa lengo la kudhibiti kuendelea kwa shughuli za kibenk.
Wakati ukisubiria uamuzi wa bunge la Cyprus katika kuamua hatima ya mpango huo wa fedha za uokozi Rais wa Urusi Vladimir Putin amekosoa vikali kwa kusema si wa haki na hakuna mfano wa hatua kama hiyo iliyowahi kutokea.
Kupitia msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, rais Putin amesisitiza kwamba mpango huo utakuwa wa hatari, usio wa haki na sio wa kitaalamu.
Idadi kubwa ya raia wa Urusi, wameweka kiasi kikubwa cha mabilioni ya euro mabenki ya Cyprus kwa utaratibu wa akaunti za kigeni, na mabenki ya urusi yamewekeza pia katika taifa hilo kibiashara.
Mwandishi: Sudi Mnette/RTR/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef