Bunge Israel kupigia kura leo mageuzi yanayoleta mgawanyiko
24 Julai 2023Hii ni hata baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kuhimiza kuahirishwa kwa mswaada huo uliosababisha mgawanyiko na miezi kadhaa ya maandamano ya umma.
Wabunge walijadili usiku kucha wakati kukiwa na juhudi za mwisho mwisho za Rais Isaac Herzog kufikia maelewano.
Alikutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu katika hospitali alikofanyiwa upasuaji wa moyo.
Netanyahu aliruhusiwa kuondoka hospitali leo na tayari yuko bungeni kwa ajili ya mchakato wa upigaji kura.
Soma pia:Maelfu waandamana kupinga mageuzi ya mahakama nchini Israel
Polisi leo wametumia mizinga ya maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji waliofunga lango la bunge.
Wakosoaji wanahofia kuwa mabadiliko ya mfumo wa mahakama yatadhoofisha demokrasia ya Israel.
Sheria hiyo inayopendekezwa itaupunguza uwezo wa majaji kuyakataa maamuzi ya serikali wanayoyaona kuwa hayafai.