Bunge la Afrika kusini lapitsha mswaada wa sheria inayobishwa
23 Novemba 2011Chama cha ANC,kilitumia wingi wa viti vyake bungeni kuidhinisha sheria inayoitwa "hifadhi ya habari za serikali"-inayotishia kumfanya mwaandishi habari ahukumie miaka mitano jela pindi akichapicha hati zinazotajikana kuwa ni za siri,au hata kifungo cha miaka 25 ikiwa mwandishi habari atakutikana na hatia ya kufanya upelelezi.
Mswaada huo wa sheria utabidi hivi sasa uwasilishwe mbele ya baraza la taifa la mikoa kabla ya kufikishwa katika ofisi ya rais Jacob Zuma kutiwa saini ifikapo mwakani.
Vyama vya upinzani vimeahidi kutuma malalamiko yao mbele ya korti ya katiba wakihoji yaliyofikiwa na bunge ni kinyume na sheria msingi ya Afrika kusini iliyoidhinishwa baada ya kumalizika enzi za ubaguzi wa rangi na amtengano-Apartheid.
Wapinzani wa mswaada huo wa sheria wanaohofia serikali nyengine barani Afrika zinaweza kuhisi njia imefunguliwa sasa kwao wao pia kupitisha hatua dhidi ya waandishi habari na wanaharakati wanaodai demokrasia.
Mswaada huo wa sheria uliolenga kuzuwia mitindo ya kueneza habari za siri umekuwa ukijadiliwa tangu mwaka 2008.
Mswaada huo wa sheria umeletwa bungeni baada ya mazungumzo kati ya wawakilishi wa chama tawala cha ANC,wawakilishi wa vyombo vya habari na wawakilishi wa mashirika ya jamii,mapema mwaka huu na kufanyiwa marekebisho kadhaa.
Shirika linalopigania haki za binaadam Amnesty International linaonya kwa kuwekea vizuwizi uhuru wa mtu kutoa maoni yake,Afrika kusini inaweza kukabwa na jinamizi baya kabisa-ambalo ni kurejea katika enzi za kale ambapo marufuku ya mtu kutoa maoni yake yalitumiwa ili kuficha visa vinavyokwenda kinyume na haki za binaadam.
Katika taarifa yake iliyochapishwa baada ya mswaada huo wa sheria kuidhinishwa,chama cha ANC kimekosoa kile walichokiita " kueneza habari ambazo si za kweli kuhusu mswaada huo wa sheria.Ni sheria kuhusu usalama na sio kuhusu vyombo vya habari" na inalingana na sheria bora kabisa zinazotumika kimataifa"-amesema mwenyekiti wa tume ya chama cha ANC inayoshughulikia masuala ya sheria Luwellyn Landers."Wanaikosoa bila ya hata kuisoma" amesisitiza.
Wapinzani wa mswaada huo wa sheria unawaleta pamoja,wakuu wa mashirika ya habari,waandishi habari,vyama vya upinzani,vyama vinavyopigania masilahi ya waandishi habari,vikiwemo vile vinavyoshirikiana na ANC,wanaharakati wa zamani wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na mtengano,na hata mshindi wa zawadi wa Nobel ya uandishi sanifu Nadine Gordimer na mshindi wa zawadi ya amani ya Nobel Desmond Tutu pamoja pia na wakfu wa Nelson Mandela.
"Ni siku ya kiza kwa uhuru wa vyombo vya habari,na siku ya kiza kwa uhuru wa mtu kutoa maoni yake-siku ya kiza pia kwa Afrika kusini-amesema Yusuf Abramjee ambae ni mwenyekiti wa shirika la taifa la vyombo vya habari na kumalizia-tutakutana mbele ya korti kuu ya katiba."
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/dpa/Afp
Mhariri: Abdul-Rahman