SiasaBrazil
Bunge la Brazil lamchagua spika chini ya ulinzi mkali
2 Februari 2023Matangazo
Mbunge anayeungwa mkono na Rais Luiz Inacio Lula da Silva, amechaguliwa kuwa spika wa bunge la Brazil jana Jumatano, akimshinda mpinzani wake ambaye amekuwa akiungwa mkono na rais wa zamani wa mrengo wa kulia, Jair Bolsonaro.
Rodrigo Pacheco anayetokea chama cha Lula anachukua wadhifa huo wa ngazi za juu katika bunge la taifa hilo la Amerika ya kusini kwa mara nyingine, baada ya ushindi wa kura 49, dhidi ya kura 32 alizozipata mpinzani wake, Rogerio Marinho wa chama cha Liberal.
Baada ya kuchaguliwa kwake, Pacheco alisema atahakikishia mkasa wa kuvamiwa majengo ya serikali uliofanywa na wafuasi wa Bolsonaro mwezi uliopita hautatokea tena. Rais Lula kupitia mtandao wake wa Twitter aliwapongeza wote wawili.