1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Congress lapitisha muswada wa kuiadhibu mahakama ya ICC

5 Juni 2024

Bunge la Marekani Jumanne limepitisha muswada utakaoipelekea Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kuwekewa vikwazo.

USA US-Repräsentantenhaus Wahlen
Bunge la MarekaniPicha: Andrew Harnik/AP Photo/picture alliance

Hii imetokana na hatua ya Mahakama ya ICC kuomba waranti wa kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wa Israel.

Muswada huo umepitishwa kwa kura 247 dhidi ya 155 za waliopinga.

Kupitishwa kwa muswada huo ni hatua ya kwanza ya bunge la Congress kuonesha kutoridhishwa kwake na hatua ya mahakama hiyo ya kutaka waranti huo wa kukamatwa kwa viongozi wa Israel, jambo lililosababisha kuwepo kwa kipindi cha nadra cha umoja kwa Israel huko Marekani, licha ya migawanyiko iliyoko kuhusiana na vita hivyo vya Israel dhidi ya kundi la wanamgambo la Hamas.

Muswada huo ulitarajiwa kupita katika Congress ila umewavutia wabunge wachache wa chama cha Democratic, jambo ambalo huenda likatilia shaka nafasi yake ya kupita katika Senate.

Ikulu ya White House inaupinga muswada huo ikisema umechupa mipaka.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW