1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

bunge la Iran laruhusu wajawazito kuharibu mimba ikilazimika

12 Aprili 2005

Teheran

Bunge la Iran limepiga kura kuruhusu utaratibu wa kuharibu mimba ikiwa hakuna njia nyengine.Sheria hiyo mpya inamruhusu mjamzito kuharibu mimba katika kipindi cha miezi minne ya mwanzo ikidhihirika kama mtoto ni mlemavu au maisha ya mama yako hatarini.Wabunge 127 kati ya 217 wameunga mkono sheria hiyo baada ya mjadala moto moto uliotangazwa moja kwa moja na radio Iran.Kabla ya mimba kuharibiwa panahitajika idhini ya wazee wote wawili,ruhusa ya madaktari watatu wa magonjwa ya wanawake pamoja na daktari mwengine wa serikali.Hadi wakati huu mitindo ya kuharibu mimba ilikua marufuku nchini Iran.Baraza la maulamaa,waalinzi wa mapinduzi ya kiislam linabidi kwanza kuidhinisha sheria hiyo.