1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Iraq lakubali uamuzi wa kujiuzulu waziri mkuu Mehdi

Oumilkheir Hamidou
2 Desemba 2019

Bunge la Iraq limeukubali uamuzi wa waziri mkuu Adel Abdul Mehd wa kujiuzulu baada ya wiki kadhaa za maandamano ya umwagaji damu dhidi ya serikali yake.

Irak Ministerpräsident Adel Abdel-Mahdi
Picha: picture-alliance/AP Photo/H. Mizban

Abdul Mehdi ameamua kujizulu baada ya kiongozi  mkuu wa waumini wa madhehebu ya Shia Ayatollah Ali al-Sistani kulitolea wito bunge ijumaa iliyopita lifikirie upya msimamo wake kuelekea serikali anayoiongoza  ili kumaliza machafuko.

 Kufuatia ridhaa hiyo ya bunge, Spika wa taasisi hiyo Mohammesd a-Halbousi amemuomba rais Barham Salih amteuwe waziri mkuu mpya" .

Wabunge wanasema serikali ya Abdul Mehdi, ikiwa ni pamoja na waziri mkuu mwenyewe, wataendelea na wadhifa wao kwa muda hadi serikali mpya itakapoteuliwa.

Kuambatana na katiba, rais Barham Salih atabidi kulishauri kundi lenye wawakilishi wengi zaidi bungeni limteue waziri mkuu mpya na kuunda serikali- hatua inayotazamiwa kudumu siku 15.

Maandamano Najaf ambako ubalozi mdogo wa Iran umetiwa motoPicha: Reuters/A. al-Marjani

 Maandamano yanaenelea licha ya waziri mkuu kujiuzulu

Vikosi vya Iraq vimewauwa karibu watu 400, wengi wao vijana, waliokuwa wakiandamana bila ya silaha kuipinga serikali tangu Oktober mosi iliyopita. Zaidi ya dazeni moja ya vikosi vya usalama wameuwawa pia katika machafuko hayo.

Uamuzi wa kujiuzulu Abdul Mehdi, ingawa waandamanaji wameukaribisha hata hivyo hauonyeshi kumaliza maandamano ambayo lengo lake ni kuachana moja kwa moja na  mfumo wa kisiasa unaotuhumiwa kuoza kwa rushwa na kuwatumbukiza wananchi walio wengi katika janga la umaskini.

Jana waandamanaji waliutia moto ubalozi mdogo wa Iran mjini Nadjaf, kwa mara ya pili katika kipindi cha wiki moja.

Maandamano yanaendelea mjini Baghdad na katika majimbo mengine ya kusini. Waandamanaji wamezifunga njia ikiwa ni pamoja na ile inayoelekea katika bandari muhimu ya kusini. Vikosi vya usalama vimemuuwa mwanaharakati mwengine mmoja na kuwajeruhi wengine tisa karibu na daraja ya mji mkuu jana.

Katika mji wa Nassiriya, waandamanaji wawili wamefariki kutokana na majaraha walioyapata kufuatia machafuko ya awali dhidi ya polisi katika mji huo wa kusini.

 

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW