1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Bunge la Israel lapinga kutambuliwa Taifa la Palestina

18 Julai 2024

Bunge la Israel limepiga kura inayopinga miito ya kutambuliwa kwa taifa huru la Palestina.

Bendera ya Dola la Palestina
Bunge la Israel lapiga kura ya kupinga Palestina kutambuliwa kama taifaPicha: picture alliance / dpa

Wabunge waliopiga kura ya kupinga kutambuliwa kwa taifa huru la Palestina ni pamoja na wanaotokea muungano wa vyama vya mrengo wa kulia unaoongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu pamoja na chama cha upinzani cha Benny Gantz.

Kura za maoni zinaonesha kuwa kina uwezekano wa kuwa chama chenye nguvu na kupata viti vingi bungeni iwapo kutaitishwa uchaguzi mpya.

Azimio hilo limeeleza kuwa kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina kunatishia uwepo wa Israel na usalama wa raia wake.

Wabunge hao wameongeza kuwa, iwapo Palestina itatambuliwa kama taifa huru, kundi la wanamgambo la Hamas litapata fursa ya kuchukua mamlaka kamili na kuigeuza Palestina kama uwanja wa itikadi kali za dini na kuratibu mashambulizi ya kigaidi kwa ushirikiano na Iran kuilenga Israel. 

Wabunge 68 kati ya 120 walipiga kura kuunga mkono azimio hilo, wabunge 9 kutoka vyama vya kiarabu walipinga azimio hilo na waliobaki waliepuka kupiga kura.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW