1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Kenya lapokea hoja ya kuuzuliwa makamu wa rais

1 Oktoba 2024

Bunge la Kenya leo limepokea hoja ya kujadiliwa inayohusu kumuondowa madarakani Makamu wa Rais Rigathi Gachagua kwa madai ya kukiuka katiba ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Makamu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua.
Makamu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua.Picha: YASUYOSHI CHIBA/AFP/Getty Images

Maelezo hayo yametolewa na spika wa bunge la nchi hiyo, wakati vyambo vya habari vya Kenya vikiripoti kwamba makamu huyo wa rais amekosana na Rais William Ruto.

Zaidi ya thuluthi moja ya wabunge wamesaini hoja hiyo iliyowasilishwa na mbunge Mwengi Mutuse anayeegemea kambi ya muungano wa Rais Ruto.

Soma zaidi: Gachagua: Idara ya Ujasusi yaifelisha serikali ya Kenya

Muungano huo unamtuhumu Gachagua, miongoni mwa mambo mengine, kwamba anawanyima watu fursa za kupata uteuzi wa nafasi za umma  na rasilimali.

Mpasuko kati ya Ruto na Gachagua umekuwa ukionekana waziwazi katika siku za hivi karibuni nchini Kenya, huku makamu huyo wa rais akisema ametengwa katika shughuli za kiserikali.