1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Bunge la Marekani laidhinisha azimio la mshikamano na Israel

26 Oktoba 2023

Hatua hiyo ilipewa jina Kusimama na Israel inapojilinda dhidi ya vita vya kikatili vilivyoanzishwa na Hamas na magaidi wengine.

Bunge la Marekani jijini Washington
Bunge la Marekani jijini Washington Picha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Wabunge wa Marekani wameidhinisha azimio la mshikamano na Israel katika vita vyake dhidi ya Hamas, hii ikiwa ni hatua ya kwanza kuchukuliwa na bunge mara baada ya kupata spika mpya wa Baraza la Wawakilishi, Mike Johnson.

Hatua hiyo iliyopewa jina "Kusimama na Israel inapojilinda dhidi ya vita vya kikatili vilivyoanzishwa na Hamas na magaidi wengine," ilipata uungwaji mkono wa karibu wabunge wote wa Republican na Democrats. Hata hivyo wabunge 10 wa Democrats hawakupiga kura.

Spika Johnson, mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Republican kutoka Louisiana, katika hotuba yake ya kukubaliwa na bunge alisema jambo la kwanza atakalofanya ni kuwasilisha muswada huo wa kuisaidia Israel.