1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Mashariki mwa Libya laidhinisha gavana mpya

30 Septemba 2024

Bunge la mashariki mwa Libya limeidhinisha uteuzi wa Najib Mohamed Issa Belqasem kuwa gavana mpya wa benki kuu ya nchi hiyo.

Abdul Hamid Dbeiba
Waziri Mkuu wa Libya, Abdul Hamid Dbeiba.Picha: Hamza Turkia/Xinhua/imago images

Uteuzi huo ulioidhinishwa siku ya Jumatatu (Septemba 30) ni sehemu ya juhudi za kuumaliza mgogoro ambao umesababisha kupungua kwa pato la mafuta nchini humo.

Katika kikao kilichooneshwa moja moja kwenye televisheni, bunge hilo pia lilimuidhinisha Mari Muftah Rahil Barrasi kama naibu gavana wa Benki Kuu.

Soma zaidi: Umoja wa Mataifa wautanzua mgogoro wa benki kuu ya Libya

Majina hayo mawili yalipendekezwa katika mkutano wa hivi majuzi uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Gavana huyo mpya hapo awali alikuwa ni mkurugenzi wa benki kuu aliyesimamia uwekaji na udhibiti wa fedha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW