1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPeru

Bunge la Peru lakataa ombi la kuitisha uchaguzi wa mapema

2 Februari 2023

Bunge la Peru limekataa pendekezo la Rais Dina Boluarte la kutaka kuitishwa uchaguzi wa mapema ili kutuliza machafuko ambayo yamesababisha vifo vya watu kadhaa katika wiki saba za maandamano ya kuipinga serikali.

ARCHIV | Peru Lima | Parlament
Picha: Luis Iparraguirre/Agentur Andina/dpa/picture alliance

Bunge la Peru limekataa pendekezo la Rais Dina Boluarte la kutaka kuitishwa uchaguzi wa mapemaili kutuliza machafuko ambayo yamesababisha vifo vya watu kadhaa katika wiki saba za maandamano ya kuipinga serikali.

Baada ya mjadala uliodumu kwa masaa matano, wabunge walipinga pendekezo la kusogeza uchaguzi hadi mwezi Desemba mwaka 2023. Ofisi ya Rais imesema haikufurahishwa na maamuzi hayo ya bunge na badala yake hivi karibuni itawasilisha muswada mwingine wa kuandaa uchaguzi mkuu mwaka huu.

Peru imeingia katika mzozo wa kisiasa na maandamano tangu Desemba mwaka uliopita, wakati rais wa wakati huo, Pedro Castillo, alipokamatwa baada ya kujaribu kulivunja Bunge.

Kulingana na ofisi ya mchunguzi wa haki za binaadamu, watu 48 akiwemo afisa wa polisi wameuwawa wakati wa makabiliano baina ya vikosi vya usalama na waandamanaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW