1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la tisa kufunguliwa leo kukiwa na matarijio juu ya serikali ya mseto kuundwa

6 Machi 2008

-

NAIROBI

Rais Mwai Kibaki leo anatarajiwa kufungua rasmi kikao cha tisa cha bunge na kufungua ukurasa mpya baada ya mazungumzo yaliyofikia makubaliano ya kuundwa serikali ya mseto.Hotuba ya rais Kibaki inatarajiwa kuelezea miongoni mwa mambo mengine sera ambazo zitatoa muongozo wa jinsi serikali hiyo mpya itakavyokuwa.

Hapo jana Polisi walifyatua gesi za kutoa machozi kutawanya maandamano yaliyokuwa yakifanywa na vija awa kundi haramu la Mungiki katika mji mkuu Nairobi.Waandamanji hao walikuwa wakidai kuachiliwa huru kutoka jela kiongozi wa kundi hilo ambalo linadaiwa kuendesha mauaji mengi nchini humo.

Kwengineko Umoja wa Mataifa umenzisha kundi maalum la wataalamu ambao watakuwa tayari kwa ajili ya kuusadia umoja huo kukabiliana na mizozo ulimwenguni kama sehemu ya harakati za kufanikisha juhudi za usuluhishi katika nchi zenye mizozo.Kundi hilo maalum lenye wanacham watano ambalo liliwatuma wanachama wake wawili wiki hii nchini Kenya litahusika katika kuwasaidia wajumbe wa Umoja wa Mataifa wanaopewa kazi ya kutatua mizozo.