1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Bunge la Ufaransa lataka Wagner litajwe "kundi la kigaidi"

10 Mei 2023

Bunge la Ufaransa lilipitisha azimio Jumanne linaloutaka Umoja wa Ulaya kuliita kundi la kampuni binafsi ya ulinzi ya Kirusi-Wagner kama kundi la kigaidi.

Mpiganaji wa kundi la Wagner akiwa nje ya majengo yaliyoharibiwa vibaya kwenye mji wa Artyomovsk, Bakhmut.
Mashambulizi katika baadhi ya maeneo nchini Ukraine yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na hata nakazi ya watu.Picha: Valentin Sprinchak/TASS/dpa/picture alliance

Mwasilisha mada, mbunge wa chama tawala nchini humo Benjamin Haddad, amesema anatumai kuwa itawahimiza mataifa wanachama 27 ya Umoja wa Ulaya kuridhia kuliweka kundi hilo Wagner kwenye orodha yake rasmi ya mashirika ya kigaidi. Kuorodheshwa kama kundi la kigaidi kunamaanisha kuwa wanachama wa Umoja wa Ulaya wanaweza kufungia mali za kundi la Wagner na wanachama wake, huku makampuni na raia wa Ulaya wakizuiwa kushughulika na wapiganaji hao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW