1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Bunge la Uingereza launga mkono wahamiaji kupelekwa Rwanda

13 Desemba 2023

Wabunge nchini Uingereza wamepiga kura ya kuunga mkono mpango wa serikali kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda, ambao umekigawa chama tawala cha Conservative, cha Waziri Mkuu Rishi Sunak.

Uingereza | Rishi Sunak
Waziri Mkuu Rishi Sunak akiwa kwenye bunge la nchi hiyo.Picha: UK Parliament/Jessica Taylor/REUTERS

Baada ya majadiliano makali, wabunge 313 walipiga kura kuridhia kile kiitwacho "Usalama wa Rwanda", muswada wa Sheria ya Kuomba Hifadhi na Uhamiaji, huku 269 wakiupinga.

Muswada huo wa dharura unachukuliwa kama jibu la Sunak kwa uamuzi wa Mahakama ya Juu ambayo mwezi Novemba ilisema kwamba kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda ni kinyume na sheria ya kimataifa.

Hata hivyo, bado kundi la wabunge wa chama chake wanaopingana na sheria hiyo, limeapa kuja na mapendekezo mapya kwa sheria mwezi ujao wa Januari, hatua inayomuweka Sunak kwenye vita vipya ndani ya Conservative.