1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ujerumani laidhinisha bajeti kubwa kwa jeshi

Hawa Bihoga
19 Oktoba 2023

Kamati ya Bajeti ya Bunge la Ujerumani imeidhinisha dola bilioni 4.64 kwa manunuzi na miradi ya maendeleo kwa jeshi la nchi hiyo, Bundeswehr.

Lettland Deutschland Verteidigungsminister Pistorius
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius.Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture-alliance

Waziri wa Masuala ya Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius, aliitaja hatua hiyo ni ishara ya kuwa wanaishi katika nyakati mpya.

Mradi mkubwa ulioidhinishwa unahusu ununuzi wa mfumo wa ulinzi wa anga kutoka Israel na karibu dola bilioni 4 ni katika fuko maalum.

Soma zaidi: Jeshi la Ujerumani linakabiliwa na ugumu wa kupata askari wapya

Kansela Olaf Scholz alisema mnamo mwezi Februari kwamba uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine vilisababisha hatua ya mageuzi na uwekezaji mkubwa katika jeshi.

Aliahidi kuongeza matumizi kwa zaidi ya asilimia mbili ya pato jumla na kuongeza Ujerumani pia itaanzisha fuko maalum litakalofadhiliwa kwa gharama za bilioni Euro 100  kwa ajili ya kuboresha jeshi lake, Bundeswehr.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW