Ujerumani haitotuma makombora ya masafa marefu Ukraine
14 Machi 2024Bunge la Ujerumani, Bundestag, limeukataa muswada huo wa upinzani kwa kura 495 kwa 190 huku kukiwa na wabunge watano ambao hawakuwepo kushiriki kura hiyo.
Upinzani ulikuwa unataka kuendelea kushinikiza kuhusiana na suala hilo na kutumia mgawanyiko ulioko katika serikali ya muungano ya Kansela Scholz.
Scholz asisitiza msimamo wake wa kutoipa Ukraine makombora ya Taurus
Hapo jana Scholz aliwaambia wabunge kwamba kukataa kwake kuchukua hatua hiyo hakumaanishi kwamba haiamini serikali ya Kyiv.
Hayo yakiarifiwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg, ameyataka mataifa rafiki kwa Ukraine katika jumuiya hiyo ya kujihami, kuipelekea silaha nchi hiyo. Stoltenberg amesema kuna haja ya dharura ya Ukraine kupelekewa silaha katika vita vyake na Urusi.